• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka 2018 wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wafunguliwa Beijing

    (GMT+08:00) 2018-09-03 17:07:14

    Mkutano wa mwaka 2018 wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika umefunguliwa leo hapa Beijing, ambapo rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba kwenye mkutano huo.

    Viongozi na wajumbe kutoka nchi 53 za Afrika, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres, mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat pamoja na wachunguzi kutoka mashirika 27 ya kimataifa na kikanda wamehudhuria mkutano huo.

    Mkutano huo wenye kauli mbiu ya "kushirikiana kwa kunufaishana, kujenga kwa pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika", utapanga sekta zinazopewa kipaumbele na mwelekeo muhimu katika ushirikiano kati ya China na Afrika katika miaka mitatu ijayo na kipindi kijacho baadaye. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako