• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono kampuni za China kushiriki kwenye ujenzi wa miundo mbinu barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-03 17:55:49

    Rais Xi Jinping wa China amesema China na Umoja wa Afrika zimeamua kuanza kupanga "Mpango wa ushirikiano kati ya China na Afrika katika ujenzi wa miundo mbinu barani Afrika", China itaunga mkono kampuni za China kuanzisha mtandao wa uwekezaji, ujenzi na uendeshaji kwa ajili ya kushiriki kwenye ujenzi wa miundo mbinu barani Afrika, na kuimarisha ushirikiano katika sekta za nishati, mawasiliano na tehema na maliasili ya maji ya kuvuka mipaka. Pia amesisitiza kuwa China itaanzisha safari nyingi zaidi za ndege za moja kwa moja kati ya China na Afrika, kuzirahisisha nchi za Afrika na mashirika yao ya fedha kuuza dhamana nchini China, na kuziunga mkono nchi za Afrika kutumia vizuri zaidi Benki ya uwekezaji wa miundo mbinu ya Asia, Benki ya Maendeleo Mapya na Mfuko wa Njia ya Hariri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako