• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono Afrika kutimiza usalama wa chakula kabla ya mwaka 2030

    (GMT+08:00) 2018-09-03 18:07:43

    Rais Xi Jinping amesema kuwa, China inaunga mkono Afrika kutimiza usalama wa chakula kabla ya mwaka 2030, kushirikiana na Afrika kutunga na kutekeleza mpango wa ushirikiano wa kilimo wa kisasa kati ya China na Afrika, kutekeleza miradi 50 ya msaada wa kilimo, kutoa msaada wa vyakula wa dharura wenye thamani ya yuan bilioni 10 kwa nchi zinazoathiriwa na maafa, kupeleka wataalamu 500 wa kilimo wa hali ya juu kuisaidia Afrika kuwaandaa vijana wenye uwezo wa kuongoza kwenye sayansi na tenkonojia ya kilimo, na wanaotangulia kujiendeleza katika kilimo.

    Amesema kuwa, China imeamua kuanzisha maonyesho ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika, kuhamasisha makampuni ya CHina kupanua uwekezaji barani Afrika, na kujenga na kuinua kiwango cha baadhi ya maeneo ya ushirikiano wa uchumi na biashara barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako