• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatarajia kujenga karakana 10 za Luban barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-03 18:09:24

    Rais Xi Jinping wa China ameahidi kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika(FOCAC) kuwa, China itajenga karakana 10 za Luban barani Afrika ili kutoa mafunzo ya ufundi wa kazi mbalimbali kwa vijana wa Afrika. Karakana za Luban ziliofunguliwa nchini Tailand na Pakistan, ni mradi wa China kutoa mafunzo ya ufundi wa kazi mbaimbali katika nchi za nje. Rais Xi amesema, China inaunga mkono kuanzisha kituo cha ushirikiano wa uvumbuzi unaolenga kuhawamasisha vijana kuanzisha shughuli zao na kufanya uvumbuzi, kitaisadia Afrika kuwaandaa wataalamu vijana 1000 wa Afrika ili wawe watangulizi wa kuongoza katika maendeleo ya Afrika. Pia China itatoa nafasi elfu 50 za udhamini wa masomo kwa Afrika, kutoa nafasi elfu 50 kwa watu wanaoshiriki kwenye semina, na kuwaalika vijana 2000 wa Afrika kuja China kufanya mawasiliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako