• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kujenga jumuiya ya mustakabali yenye uhusiano wa karibu zaidi na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-03 18:09:43

    Rais Xi Jinping wa China leo amesema kwenye mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, China inapenda kushirikiana na Afrika kujenga jumuiya yenye mutakabali wa pamoja inayobeba majukumu kwa pamoja, kufanya ushirikiano wa kunufaishana, kusitawisha pamoja tamaduni, kujenga mazingira ya usalama kwa pamoja na kuishi pamoja katika hali ya masikilizano. China na Afrika zinapaswa kufanya mazungumzo ya kisiasa na kubadilishana mawazo kuhusu sera katika ngazi mbalimbali, kupanua nafasi mpya za ushirikiano, kuharakisha kuandaa kazi zitakazoleta ongezeko katika sekta ya uchumi mpya, kuwaletea watu wa China na Afrika matunda na manufaa halisi, kupanua mawasiliano kati ya watu wa sekta za utamaduni, sanaa, elimu na michezo, kuunga mkono kithabiti nchi za Afrika na Umoja wa Afrika kutatua masuala ya Afrika kwa njia ya Afrika na kuimarisha maingiliano na ushirikiano katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na matatizo mengine katika kulinda mazingira ya asili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako