• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inaunga mkono nchi za Afrika kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kunufaika na matunda yake

    (GMT+08:00) 2018-09-03 19:11:45

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amehudhuria mkutano wa ngazi ya juu wa viongozi na wadau wa viwanda na biashara kati ya China na Afrika, na ufunguzi wa mkutano wa 6 wa wajasiriamali kati ya China na Afrika. Katika hotuba yake, rais Xi amesisitiza kuwa China inaunga mkono nchi za Afrika kushiriki kwenye ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na inapenda kufanya kazi na Afrika katika kuunganisha mikakati yao, na kujenga njia ya kujiendeleza ya kiwango cha juu inayoendana na hali halisi ya nchi husika. …………….. na maelezo zaidi:

    Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi 35 wa nchi za Afrika wanaoshiriki kwenye mkutano wa kilele wa FOCAC unaofanyika hapa Beijing, wajasiriamali mashuhuri wa China na Afrika na wajumbe wa mashirika ya kimataifa wapatao elfu moja. Rais Xi amesisitiza kuwa, watu wa Afrika ni moja ya sita ya watu wote duniani, na kujiendeleza kwa pamoja kwa watu wote duniani wakiwemo watu wa Afrika, ni sehemu muhimu ya kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Amesema China na Afrika ni marafiki wa muda mrefu, na ni ndugu wazuri waliopambana na maadui kutoka nje bega kwa bega, na sasa ni wenzi wazuri wanaotafuta maendeleo kwa pamoja. Rais Xi pia amesema Afrika ni mshiriki muhimu katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa mujibu wa historia na jiografia,

    "China inaunga mkono nchi za Afrika kushiriki kwenye ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Katika msingi wa usawa na kusaidiana, na kufuata kanuni za kushauriana, kujenga kwa pamoja na kunufaishana, China inapenda kushirikiana na Afrika katika kuunganisha mikakati yao, kuhimiza uratibu wa sera, kuunganishwa kwa vifaa, kuhakikisha biashara inafanyika kwa utaratibu, mafungamano ya kifedha na maelewano kati ya watu, na kujenga njia ya kujiendeleza ya kiwango cha juu inayoendana na hali halisi ya nchi husika, inayowashirikisha na kuwanufaisha watu wote, kusaidiana na kunufaishana."

    Rais Xi amesema huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Bila ya kujali mabadiliko ya hali ya kimataifa, China itaendelea kufungua mlango bila ya kusita, na kwa uwazi zaidi. Pia Rais Xi amesema China inawakaribisha wajasiriamali wa nchi mbalimbali wakiwemo kutoka Afrika kufanya shughuli za biashara nchini China, na pia kuwahamasisha wajasiriamali wa China kwenda Afrika kutafuta fursa za kujiendeleza ili kushirikiana kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Amesema,

    "Tunatumai wajasiriamali wa China na Afrika watabeba majukumu ya kijamii, kuheshimu utamaduni na desturi za nchi wanazoishi na kufanya kazi, kuzingatia kuinua sifa ya kampuni, kutilia maanani kazi za kutoa mafunzo kwa wafanyakazi na kuboresha maisha ya wakazi wazawa, kutilia maanani uhifadhi wa mazingira na kubana matumizi ya maliasili ili kujenga mazingira mazuri kwa maendeleo ya muda mrefu. Pia, kujichukulia kama ni daraja la urafiki kati ya China na Afrika katika ushirikiano wa kiuchumi, kupanda mbegu ya urafiki katika sehemu wanapofanya biashara na kujenga mnara wa urafiki mahali miradi inapotekelezwa."

    Rais Cyril Ramaphosa ambaye anashiriki kwenye mkutano huo amesema, mipango 10 ya ushirikiano iliyotangazwa kwenye mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini mwaka 2015 ulihimiza kwa nguvu kubwa maendeleo ya pande zote ya uchumi na jamii ya Afrika.

    "Mipango 10 ya ushirikiano iliyotangazwa kwenye mkutano wa kilele wa FOCAC mjini Johannesburg imepongezwa na nchi mbalimbali za Afrika, hatua hizo zimeunganishwa na mambo yaliyopewa kipaumbele na nchi za Afrika. Kinachotutia moyo ni kwamba, thamani ya biashara kati ya Afrika na China imefikia dola za kimarekani bilioni 170, uwekezaji wa China barani Afrika kati ya mwaka 2000 hadi mwaka 2017 umezidi dola za kimarekani bilioni 100, ujenzi wa reli zenye urefu wa kilomita 6500, barabara yenye umbali wa kilomita 6000, vituo 70 vya uzalishaji wa umeme, bandari 20 na shule 200. Hayo ni mafanikio makubwa."

    Viongozi wengi wa Afrika wanaohudhuria mkutano huo wanaona kuwa, Afrika inatarajia mkutano huo wa kilele wa Beijing utashiriki kwa kina ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kushirikiana na China kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya China na Afrika yenye karibu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako