• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafanya juhudi kujenga Jumuiya yenye hatma ya pamoja iliyo karibu zaidi kati yake na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-03 20:01:34

    Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika ulioanza leo hapa Beijing.

    Katika hotuba hiyo, rais Xi amesema katika miaka mitatu ijayo na kipindi kifuatacho, China itajenga Jumuiya yenye hatma ya pamoja kati yake na Afrika iliyo ya karibu zaidi kwa njia ya kutekeleza mipango katika sekta nane zikiwemo kuhimiza maendeleo ya viwanda, ujenzi wa njia za mawasiliano, kurahisisha njia za kufanya biashara, na maendeleo yasiyo na uchafuzi wa mazingira. Hili ni wazo jipya na hatua mpya zinazotolewa na China inayotupia macho siku za mbele, ambalo limeweka mipango wa maendeleo kuhusu uhusiano kati ya China na Afrika.

    Akiwa ziarani barani Afrika miaka mitano iliyopita, rais Xi alisema "China na Afrika siku zote ziko kwenye Jumuiya yenye hatma ya pamoja". Tangu Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika lilipoanzishwa mwaka 2000, thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili imeongezeka mara 17, huku uwekezaji wa China barani Afrika ukiongezeka mara 100. Hii imefanya ushirikiano wa kunufaishana na kutafuta maendeleo ya pamoja kuwa kanuni muhimu inayoelekeza uhusiano kati ya pande hizo mbili katika karne ya 21.

    Hivi sasa hali ya dunia imebadilika, vitendo vya kujilinda kibiashara na utaratibu wa upande mmoja vinaibuka, huku hali ya ukosefu wa utulivu na kutoweza kutabirika inakabili maendeleo ya nchi duniani. Kutokana na hali hii, China ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, na Afrika likiwa bara linalojumuisha nchi nyingi zaidi zinazoendelea duniani, zina hamu na mahitaji makubwa ya kuimarisha ushirikiano, na pia zinapaswa kubeba jukumu la kushirikiana kulinda biashara huria duniani, na utaratibu wa pande nyingi. Ni mahitaji ya sasa ya kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika iliyo na karibu zaidi, na kuunganisha vizuri zaidi maendeleo ya China na msukumo wake katika kuhimiza maendeleo ya Afrika.

    Katika hotuba hiyo, rais Xi pia amesisitiza kuwa China inashikilia miiko mitano katika ushirikiano kati ya China na Afrika: kutoingilia kati juhudi za nchi za Afrika katika kutafuta njia ya kujiendelea kwa kufuata hali halisi, kutoingilia kati mambo ya ndani ya Afrika, kutoweka matakwa yake kwa nguvu kwa nchi nyingine, kutoweka masharti yoyote ya kisiasa katika ushirikiano na Afrika, wala kutojitafutia maslahi ya kisiasa katika uwekezaji na mchanganyiko wa fedha barani Afrika.

    Rais Xi amesema, China itatangaza mipango minane ili kutimiza lengo hilo, na inapenda kutoa msaada wa dola za kimarekani bilioni 60 barani Afrika kwa njia ya misaada kwa serikali, uwekezaji na uchangishaji wa fedha wa mashirika ya kifedha na kampuni. Mipango hiyo itatekelezwa kwa kufuata kanuni tatu: Kushikilia kipaumbele cha maslahi ya watu wa China na Afrika; Kuisaidia Afrika kuongeza uwezo wa kujiendeleza na kuimarisha uoanishaji wa mikakati ya maendeleo.

    Tangu Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika lilipoanzishwa miaka 18 iliyopita, ushirikiano kati ya pande hizo mbili umepiga hatua katika njia mpya ya kupata manedeleo kwa pamoja, ambayo imekuwa mfano mzuri katika kujenga Jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Hivi sasa ushirikiano kati ya China na Afrika uko kwenye mwanzo mpya, na "kukabiliana na hatma kwa pamoja na kutafuta maendeleo ya pamoja" ni chaguo la pamoja la pande zote mbili katika kukabiliana na maudhui ya amani na maendeleo kwa hivi sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako