• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • BOT yapongezwa kwa kuhakikisha uchumi hauyumbi

    (GMT+08:00) 2018-09-03 20:36:19

    Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein ameeleza kuvutiwa kwake na mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hasa katika kuhakikisha uchumi hauyumbi.

    Shein amesema jitihada kubwa zimechukuliwa na BoT ambazo zimesaidia kwa kiwango kikubwa kuimarisha uchumi na kuunga mkono juhudi za Serikali.

    Aliongeza kuwa mikakati na juhudi zinazochukuliwa na BoT kwa sasa ni kuhakikisha mzunguko wa fedha unakuwepo hasa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi, jambo ambalo ni la busara na litasaidia kwa kiwango kikubwa kukuza maendeleo ya uchumi wa Tanzania na wananchi wake. Amesisitiza kuwa BoT ambayo imepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake ni ya wananchi wote Watanzania kwa ujumla hivyo ni vyema wakafaidika na huduma zake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako