• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: India yaidhinisha mfumo wa ushirikiano wa biashara kati yake na Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-09-03 20:38:02

    Serikali ya India imeidhinisha mfumo wa ushirikiano wa biashara kati yake na Rwanda ili kuwezesha mahusiano bora ya kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

    Mfumo huo ulisainiwa Julai 23 mwaka huu wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi nchini Rwanda.

    Mfumo unatarajiwa kuboresha biashara kati ya nchi hizo mbili kwa manufaa ya pamoja.

    Mnamo Julai, wakati wa ziara yake, Modi aliambatana na zaidi ya wawekezaji 100 wa sekta binafsi kutoka maeneo mbalimbali ili kuchunguza fursa za ushirikiano wa biashara na kiuchumi.

    Kwa sasa mauzo ya nje ya Rwanda kwenda India ni pamoja n alumini hasa, mbolea na bidhaa za maziwa huku pia RwandaAir, ikifanya ziara mara nne kila wiki kwenda Mumbai.

    Miradi ya uwekezaji kutoka Indianchini Rwanda imeongezeka kutoka 66 mwaka jana hadi 91 mwaka huu hasa kwenye sekta za ICT, viwanda na usindikaji wa bidhaa za kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako