• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda yaiomba Tanzania kuongeza masaa ya kazi mpakani

    (GMT+08:00) 2018-09-03 20:38:28

    Uganda imeiomba Tanzania kuwa na oparesheni za masaa 24 kwenye mipaka yake huku Uganda ikilalamika kuwa muda wa masaa manane ya biashara katika mipaka ya nchi hizo hautoshi.

    Kulingana na ripoti iliotolewa na wawakilishi wa kudumu kuhusu mipaka ya nchi hizo mbili, masaa manane kwa upande wa Tanzania huzuia mtiririko biashara.

    Kwa mujibu wa ripoti hiyo, eneo la mpaka la Mutukula nchini Uganda tayari linaendesha operesheni ya saa 24 wakati upande wa Tanzania unafanya kazi kwa masaa manane tu.

    Nchi hizo mbili zinajadii njia za kutatua tofauti za biashara katika ngazi zote, ikiwa ni pamoja na masuala yanayojitokeza ambayo yanazuia mahusiano ya nchi zote.

    Waziri wa mambo ya kigeni wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga, amesema masuala yaliyotolewa, hasa yaliyopendekezwa na Uganda, yatatatuliwa ndani ya miezi sita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako