• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Mwanariadha wa Kenya ashinda mbio Ulaya bila kiatu

  (GMT+08:00) 2018-09-04 09:39:58

  Licha ya kiatu kimoja kumvuka mwanariadha wa Kenya Conseslus Kipruto amechukua ubingwa wa mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji katika ligi ya almasi ya IAAF Diamond League mjini Zurich, nchini Switzerland.

  Mwanariadha huyo baada ya kupiga kona moja ya uwanja kiatu chake cha kushoto kilitoka lakini hilo halikumzuia kuendelea na shindano hilo na kumpita Soufiane El Bakkali katika mita za mwisho baada ya kuruka kiunzi cha mwisho akiwa wa pili.

  Wakenya katika mitandao ya kijamii ikiwemo naibu rais William Ruto wamekuwa wakimpongeza Kipruto kwa ushindi huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako