• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China aandaa tafrija kwa viongozi wanaohudhuria mkutano wa kilele wa FOCAC

    (GMT+08:00) 2018-09-04 10:09:49

    Rais Xi Jinping wa China na mke wake Bi. Peng Liyuan jana usiku waliandaa tafrija ya kuwakaribisha viongozi wa kigeni na wanandoa wao ambao wapo Beijing kuhudhuria mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Kwenye tafrija hiyo Rais Xi alisema, kwa miaka 12 iliyopita viongozi wa China na Afrika walikusanyika mjini Beijing kuimarisha urafiki na kujadili ushirikiano, hivi sasa pande hizo mbili zinasisitiza matumaini yao ya mwanzo, na kuendelea na majukumu yao na kujenga mustakabali mzuri wa pamoja. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi za Afrika kutekeleza ahadi na kuandika historia kwa vitendo, ili watu wa China na Afrika wataishi maisha bora zaidi na urafiki kati ya pande hizo mbili utafurahia mustakbali mzuri zaidi.

    Kwa niaba ya nchi za Afrika, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema FOCAC imetoa fursa muhimu kwa ushirikiano kati ya Kusini na Kusini na ushirikiano kati ya pande nyingi, na China ni mwenzi mwaminifu wa nchi za Afrika katika kutimiza lengo la ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako