• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China ahutubia ufunguzi wa Mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC

    (GMT+08:00) 2018-09-04 10:49:22

    Tarehe 3 Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika umefunguliwa kwa shangwe kwenye Jumba la mikutano ya umma la Beijing. Rais Xi Jinping wa China alihudhuria ufunguzi wa mkutano na kutoa hotuba isemayo "Tushirikiane kwa kuelekea mustababali wetu wa pamoja na kuhimiza maendeleo kwa moyo mmoja", akisisitiza kuwa China na Afrika ni lazima zipeane mikono ili kujenga pamoja Jumuia ya mustakabali wa pamoja wa China na Afrika ambapo pande mbili zibebe majukumu kwa pamoja, kufanya uhirikiano wa kunufaishana, kufaidika pamoja na matunda pamoja, kusitawisha utamaduni pamoja, kujenga mazingira ya usalama kwa pamoja, na kuishi pamoja kwa masikilizano; na China na Afrika zitaweka mkazo katika vitendo vikubwa vinane vya kuhimiza maendeleo ya viwanda, kufungamanisha miundombinu, kurahisisha biashara, kujiendeleza bila kuchafua mazingira, kujenga uwezo, kutilia maana afya na matibabu, kufanya mawasiliano ya utamaduni, na kudumisha amani na usalama.

    Rais Xi amedhihirisha kuwa, kutokana na historia zilizo za kufanana na majukumu ya pamoja, pande mbili za China na Afrika zilisonga mbele pamoja kwa moyo mmoja, zilifuatiliana na kusaidiana, na kufuata njia yenye umaalumu dhahiri ya kufanya ushirikiano wa kunufaishana. Kwenye njia hii, China siku zote inafuata mtazamo wa kushikamana na nchi mbalimbali za Afrika kikweli, kihalisi, kirafiki na kidhati, na kufuata mtazamo wa kuzingatia maadili na faida, lakini maadili yanatangulia, huku zikiungana mkono, kusaidiana na kushirikiana katika njia ya kusonga mbele. Katika ushirikiano huo, Chhina inashikilia kuwa na udhati na urafiki, kutendeana kwa usawa, kushikilia kufuata maadili kwanza halafu kuzingatia faida, kushikilia kujiendeleza kwa ajili ya wananchi, kufuata hali halisi ili kupata ufanisi mkubwa, na kushikilia kufungua mlango na kushirikiana na pande nyingi ili kusonga mbele kwa pamoja. China imeshikilia miiko mitano yaani kutoingilia kati nchi za Afrika kufanya utafiti ili kutafuta njia za kujiendeleza kwa kulingana na mazingira yao, kutoingilia kati mambo ya ndani ya Afrika, kutoilazimisha ipokee nia yake yenyewe, kutoongeza sharti lolote la kisiasa katika utoaji wa msaada kwa Afrika, na kutojitafutia faida binafsi katika kuwekeza vitega uchumi na kukusanya mitaji barani Afrika. China ina matumaini kuwa nchi mbalimbali duniani zitaweza kushikilia pia miiko hiyo mitano katika kushughulikia mambo ya Afrika.

    Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, maendeleo ya Afrika ni yasiyo na ukomo, mustakabali wa Afrika unajaa matumaini, urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika una mustakabali mpana. Uhusiano wa wenzi wa kimkakati na ushirikiano kati ya China na Afrika utawahamasisha watu wawe na nia thabiti na hamasa kubwa zaidi za kutekeleza majukumu kwa pande zote. China daima ni rafiki mzuri, mwezi mzuri na ndugu mzuri wa Afrika. Ushirikiano kati ya China na Afrika ni mzuri au la, ni watu wa China na Afrika tu ndiyo wanayo haki ya kutoa sauti. Mtu yeyote haruhusiwi kuharibu mshikamano mkubwa wa watu wa China na Afrika, mtu yeyote atashindwa kuzuia watu wa China na Afrika wasipige hatua mbele kwa kujiendeleza, na mtu yeyote atashindwa kukanusha kwa anavyodhani na kwa mtazamo wake mmoja mafanikio dhahiri yaliyopatikana katika ushirikiano kati ya China na Afrika, na mtu yeyote atashindwa kuzuia na kusumbua jumuiya ya kimataifa kwa juhudi zake za kuunga mkono kujiendeleza kwa nchi za Afrika.

    Rais Xi Jinping amedhihirisha kuwa, amani na maendeleo ni maudhui pia ni somo kuu kwa zama hizi, ndiyo maana China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali duniani katika kujenga Jumuia ya mastakabali wa pamoja ya binadamu, inapenda kujenga pamoja na wenzi wake wa ushirikiano duniani "Ukanda mmoja, njia moja" ili kujenga "Ukanda mmoja, njia moja" kuwa njia ya amani, njia ya usitawi, njia ya kufungua mlango, njia ya kujiendeleza bila kuchafua mazingira, njia ya kufanya uvumbuzi na njia ya ustaarabu.

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini ambayo ni nchi mwenyekiti mwenzi wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, Rais Paul Kagame wa Rwanda, nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika, wageni waheshimiwa waalikwa, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki walitoa hotuba pia wakisema, urafiki wa jadi wa Afrika na China ni mkubwa, matunda ya ushirikiano wa kirafiki ni kemkem. Katika muda mrefu uliopita, Afrika na China zimefanya ushirikiano wa kufuata hali halisi kwenye msingi wa kuwa na usawa, kuheshimiana na kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja. Na China imetoa uungaji mkono kwa nguvu kubwa kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na jamii ya Afrika, China haiingilii kati mambo ya ndani ya Afrika na kutoongeza sharti lolote la kisiasa katika ushirikiano wake na Afrika. Nchi za Afrika zinapinga watu wale kwa hoja yao ya ati "ukoloni mambo leo" iliyozushwa nao kwa sababu hawataki kuona ushirikiano kati ya China na Afrika. Upande wa Afrika unasifu sana pendekezo la kujenga pamoja "Ukanda mmoja, njia moja", nchi za Afrika zinapenda kushiriki na kufanya ushirikiano katika ujenzi husika, na kuufungamanisha na ujenzi wa Afrika ili kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako