• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Uchakachuaji wa mafuta wapungua Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-09-04 19:25:14

    Programu ya kuweka vinasaba kwenye mafuta imepunguza uchakachuaji kutoka asilimia 78 ya mwaka 2007 hadi kufikia pungufu ya asilimia nne kufikia mwisho wa mwaka 2017.

    Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Profesa Jamidu Katima ameyasema hayo alipokuwa akilezea mambo ambayo mamlaka hiyo imetekeleza kwa mafanikio kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma iliyokuwa chini ya mwenyekiti wake Dk Raphael Chegeni.

    Amesema programu ya kuweka vinasaba kwenye mafuta yote yanayotumika nchini ilianza Septemba 2010 kwa lengo la kuleta usawa katika ushindani na kuhakikisha ubora wa mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako