• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rais wa Rwanda apongeza uhusiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-04 19:29:58

    Rais wa Rwanda Paul Kagame ameutaja uhusiano uliopo kati ya China na Afrika kama uliojengwa chini ya misingi ya usawa, kuheshimiana na kujitolea kwa ustawi wa pamoja.

    Kagame ameyasema hayo wakati akihutubia viongozi kutoka Afrika na China kwenye Mkutano wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaoendelea katika mji mkuu wa China, Beijing.

    Mkutano huo, wa saba wa aina yake, ni jukwaa ambapo nchi zote za Afrika na China hukutana mara kwa mara ili kuona jinsi ya kuimarisha uhusiano kwa pamoja kwa lengo la kujenga maendeleo ya baadaye kwa pamoja.

    Rais Kagame alisema mkutano huo umekuwa injini yenye nguvu ya ushirikiano, na unaendana kikamilifu na Agenda ya 2063 ya Afrika na Malengo ya Maendeleo Endelevu.

    Wakati wa mkutano huo China imetangza kuwa itatoa dola bilioni sitini kwa bara la Afrika kama mikopo, misaada na uwekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako