• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: TBS yasisitiza uhakiki wa ubora wa bidhaa

    (GMT+08:00) 2018-09-04 19:33:21

    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dk Ngenya Athuman amesema bado kuna bidhaa nyingi zilizo kwenye kundi la lazima kuthibitishwa, zilizoingia sokoni bila ubora wake kuhakikiwa.

    Aliyasema hao wakati wa ufunguzi wa semina kwa wajasiriamali 60 kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Katavi, Kigoma na Tabora na kuongeza kuwa hali hiyo inafanya kuwapo na bidhaa ambazo ubora wake una mashaka.

    Alisema kuwapo sokoni kwa bidhaa ambazo ziko kwenye kundi la lazima kuthibitishwa na hazijafanya hivyo kunatelea ushindani usio sawa.

    Alisema TBS ilitoa takribani miezi mitano kuanzia Agosti hadi Desemba kwa wajasirimali kuthibitisha viwango na ubora wa bidhaa zao na kuwa baada ya hapo watafanya operesheni za kuondoa sokoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako