Wadau wa sekta ya uchukuzi wa ndege barani Afrika wanatarajiwa kukutana nchini Kenya wiki ijayo kujadili usimamizi wa sekta hiyo huku Umoja wa Afrika ukiendelea kusuuma ajenda ya kuwa na anga huru barani humo.
Mkutano huo utakaoandaliwa na Shirika la Huduma za Usafiri wa anga na utaleta pamoja wakuu wa mashirika uya ndege kutoka zaidi ya nchi 30 za Afrika.
Mkuu wa mamlaka ya usafiri wa anga nchini Kenya Gilbert Kibe amesema watajadili lengo la Afrika la kufikia mfumo wa usafiri salama wa anga, utaalum, na ushindani wa gharama nafuu.
Mkutano huo utafanyika chini ya wenyekiti wa Hamza Johari, ambaye ni mkurungezi wa mamlaka ya usafiri wa anga nchini Tanzania.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |