• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashaka ya nchi za magharibi hayatazuia ushirikiano wenye ufanisi mkubwa kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-04 19:47:01

    Mkutano wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaendelea hapa mjini Beijing. Katika miaka 18 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Baraza hilo, kumekuwa na mashaka na kupaka matope ushirikiano kati ya pande hizo mbili, lakini hata hivyo, ushirikiano kati ya China na Afrika umepiga hatua thabiti na kupata matunda mazuri. Wakati huo huo baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za magharibi na washauri bingwa ambao walitilia shaka juu ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili wametoa ripoti inayoonesha ukweli wa mambo.

    Mwaka 2015 mradi wa utafiti kuhusu mambo ya Afrika wa Chuo kikuu cha John Hopkins cha Marekani ulitoa ripoti ikisema, kuna uwezekano kuwa nchi za Afrika hazitaweza kulipa mikopo ya China, lakini ripoti iliyotolewa hivi karibuni na mradi huo inaona kuwa, mikopo ya China si chanzo kikubwa cha madeni ya nchi za Afrika, kwani madeni ya Afrika yanatoka kwenye mashirika mbalimbali ya kimataifa ya fedha, na hayatolewi na upande mmoja pekee.

    Shirika la habari la Marekani CNN hivi karibuni limeinukuu ripoti iliyotolewa na kampuni ya ushauri ya McKinsey kuwa, China imetoa nafasi milioni kadhaa za ajira barani Afrika, na theluthi mbili ya kampuni za China zimeandaa mafunzo ya ufundi kwa wafanyakazi wa huko.

    Shirika la habari la Uingereza BBC limemnukuu Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Bw. Akinwumi Adesina akisema, ingawa watu wengi wana wasiwasi na China, lakini kwa maoni yake anaona kuwa China ni rafiki wa Afrika. Vilevile imemkariri mtaalamu wa uwekezaji wa Ghana Bw. Michael Kottoh akisema, Afrika imepata matokeo halisi katika ushirikiano na China katika sekta za biashara, uwekezaji na fedha, na miradi hiyo haina masharti ambayo yaliwekwa na nchi za Afrika katika historia ya ushirikiano.

    Maneno hayo ya Bw. Kottoh yamethibitisha kanuni za miiko mitano inayoshikiliwa na China katika ushirikiano kati yake na Afrika, ambayo ni kutoingilia juhudi za nchi za Afrika katika kutafuta njia ya kujiendeleza inayoendana na hali halisi; kutoingilia mambo ya ndani ya nchi za Afrika; kutolazimisha nchi za Afrika kupokea masharti yake; kutoweka masharti yoyote ya kisiasa katika misaada kwa Afrika; wala kutojitafutia faida za binafsi katika uwekezaji na mchanganyiko wa fedha barani Afrika. Mkutano wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika umeonesha hatua za pamoja za China na Afrika katika mchakato wa kujenga Jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja wakati wa mchakato wa mageuzi chini ya utaratibu wa kushughulikia mambo ya dunia nzima. Ushirikiano kati ya China na Afrika ni msukumo muhimu katika kupaza sauti ya nchi zinazoendelea, kuboresha utaratibu wa kimataifa na kuhimiza mageuzi ya utaratibu wa kushughulikia mambo ya dunia, na pia kuweka mfano mazuri kwa ushirikiano kati ya pande nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako