• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Ramaphosa Apongeza Hotuba Ya Rais Xi Jinping na Mafanikio Ya Mkutano Wa Focac Wa Beijing

    (GMT+08:00) 2018-09-05 08:33:23

    Rais wa Afrika Kusini Cyrill Ramaphosa amepongeza hotuba ya Rais Xi Jinping aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika na kusema inatoa imani kubwa ya maendeleo ya pamoja kati ya China na Afrika katika siku zijazo.

    Aidha Rais Ramaphosa amesema pendekezo alilotoa Rais Xi Jinping la kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu ni thabiti ambalo litaimarisha zaidi ushirikiano wa kivitendo kati ya watu wa China na watu wa Afrika.

    "Huu ni mtazamo wa kupiga hatua katika siku zijazo na unaolenga zaidi maendeleo ya pamoja, kupitia utekelezaji thabiti wa mapendekezo na mipango iliyowekwa, inayozingatia ushirikiano wa kivitendo kati ya watu wa pande mbili za ushirikiano. Pia, Kwa kuwa China imepiga hatua ya kimaendeleo nchi za Afrika zitajifunza zaidi uzoefu, lakini vile vile kuna baadhi ya nchi za Afrika ambazo zimepata maendeleo ya kisekta ambayo China itahitaji kujifunza. Lakini zaidi kwa vijana ambapo China imetoa fursa kwa vijana wengi zaidi kupata elimu na mafunzo ya maarifa mbalimbali nchini China."

    Katika hatua nyingine Bw. Ramaphosa amesema mkutano wa FOCAC wa mwaka huu wa hapa Beijing umefanyika kwa mafanikio makubwa, ukiwa umeandika historia mpya, na kwamba umefungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika.

    Akisema idadi kubwa ya miradi imeorodheshwa, na makubaliano mengi yamesainiwa, hivyo bara la Afrika limepata mshirika ambaye ni mzuri, aliye tayari kusaidia ukuaji wa pamoja.

    "Tulikuwa na Vongozi wengi zaidi wa nchi za Afrika pamoja na Rais Xi Jinping, jambo ambalo limeonyesha kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika umeingia katika zama za dhahabu, zama ya ushirikiano imara zaidi, wenye manufaa kwa pande zote, ushirikiano wa usawa, ushirikiano wa kuheshimiana na uliojengwa kwenye misingi ya historia."

    Vile vile Bw. Ramaphosa amekosoa vikali hatua ya nchi zinazohimiza kujitenga kibiashara, na kuzitaka zifuate utaratibu unaofuatiliwa kwa pamoja na jumuiya ya kimataifa, hivyo amezionya nchi za Afrika kujiepusha na vitendo vya kujitenga.

    "Mazingira ya duniani kwa sasa yanakumbana na changamoto nyingi zinazotokana na misingi ya kisiasa, hasa kwa nchi zenye mawazo ya kujilinda zenyewe, jambo ambalo ni kinyume na kanuni zinazoongoza jumuiya ya kimataifa kwa kuzingatia makubaliano ya pamoja. Hivyo ni vyema tukawa waangalifu na wenye kuzingatia kufanya kazi pamoja kuliko kujitenga."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako