• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi akutana na marais wa Kenya na Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-09-05 08:45:23

    Rais Xi Jinping wa China jana alikutana na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na wa Rwanda Paul Kagame waliohudhuria mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika hapa Beijing.

    Kwenye mkutano wake na rais Kenyatta, rais Xi alisema ushirikiano wa kina na wa kimkakati umeleta maendeleo makubwa na kupelekea ushirikiano katika nyanja mbalimbali. Amesisitiza kuwa China iko tayari kuimarisha ushirikaino kati ya vyama na kupeana uzoefu wa kiutawala na Kenya, kupanua ushirikiano katika maeneo ya kilimo, ujenzi wa miundo mbinu, huduma za afya pamoja na ujenzi wa kiviwanda, na kuisaidia Kenya kufikia Ajenda ya Big Four.

    Adha alipozungumza na mwenzake wa Rwanda, rais Xi alimshukuru rais Kagame kwa kuhudhuria mkutano, na pia kama mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika na mchango wake katika kufanikisha mkutano. Amesema ushirikiano wa kina wa watu wa Afrika na China umefanya viongozi wengi wa Afrika kuja kuhudhuria mkutano wa kilele.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako