• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waandishi wa habari pamoja na marais wa nchi wenyekiti wenza wa Afrika wa FOCAC

    (GMT+08:00) 2018-09-05 09:12:55

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na waandishi wa habari pamoja na rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na rais Macky Sall wa Senegal ambao ni marais wa nchi mwenyekiti aliyepita na wa sasa wa Afrika wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Mwaka 2018 wa FOCAC.

    Rais Xi ametangaza kuwa Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Mwaka 2018 umemalizika kwa mafanikio kwa kutoa Azimio la Beijing—"Kuelekea kuwa Jumuiya yenye nguvu zaidi kati ya China na Afrika ikiwa na Mustakbali wa Pamoja, ambalo limedhihirisha makubaliano kati ya pande hizo mbili kuhusu masuala makuu ya sasa ya kimataifa na kikanda, na kutoa ishara yenye nguvu kwa dunia kuwa China na Afrika zinasonga mbele bega kwa bega.

    Rais Xi amesema Mpango wa Utekelezaji wa Beijing wa FOCAC wa kuanzia mwaka 2019 hadi 2021 pia umepitishwa katika mkutano huo wa kilele na kuthibitisha kuwa China na Afrika zitaimarisha kwa pande zote ushirikiano wa kivitendo unaoangalia utekelezaji wa mapendekezo manane makuu.

    Rais Xi amesema nchi zote wanachama wa FOCAC zimekubaliana kujenga kwa pamoja jumuiya ya China na Afrika yenye Mustakbali wa Pamoja inayobeba wajibu wa pamoja, kutafuta ushirikiano wa kuleta maendeleo kwa pamoja, kuleta furaha kwa watu wote, kufurahia ustawi wa kitamaduni kwa pamoja, kuhakikisha usalama wa pamoja na kuhimiza mapatano kati ya binadamu na maumbile, jambo ambalo litatoa mfano kwa ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Nchi zote wanachama wa FOCAC zimekubaliana kuwa uhusiano kati ya China na Afrika ni wa ushirikiano unaotafuta maendeleo kwa pamoja na uko katika kipindi kizuri cha historia.

    Rais Xi amesema China na nchi za Afrika zinapenda kuzidi kuunganisha na kuratibu mikakati na sera zao, kusukuma mbele maendeleo ya pamoja ya Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuunganisha pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika, Ajenda 2030 ya Umoja wa Mataifa kwa Maendeleo Endelevu na mikakati ya maendeleo ya nchi za Afrika.

    Rais Xi amesema nchi zote wanachama wa FOCAC pia zimekubaliana kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika ni sehemu ya ushirikiano wa kimataifa na Afrika. Katika kushirikiana na Afrika, nchi zote za jumuiya ya kimataifa zinapaswa kuheshimu mamlaka ya nchi za Afrika, kusikiliza sauti za Afrika, kuzingatia kwa makini utetezi wa Afrika na kufuata ahadi zilizotolewa kwa Afrika.

    Rais Xi ameongeza kuwa mafanikio ya mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC yameinua uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kwenye ngazi mpya ya kihistoria na kuanza safari mpya.

    Marais Ramaphosa na Sall wamesema FOCAC iliyoanzishwa miaka 18 iliyopita imekuwa jukwaa zuri kwa nchi za Afrika kuongeza kasi ya maendeleo, na nchi za Afrika zinashukuru juhudi za China za kuchangia maendeleo ya Afrika. Matunda mbalimbali yaliyopatikana kwenye mkutano huo wa kilele yameonesha urafiki mkubwa wa kindugu kati ya Afrika na China na pia kupanga mustakbali mzuri wa maendeleo ya uhusiano kati ya Afrika na China. Nchi za Afrika zinapenda kushirikiana na China, kuimarisha uhusiano wao, kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kutekeleza vizuri hatua mpya za ushirikiano kati ya pande hizo mbili, kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika iliyo ya karibu zaidi ili kuwanufaisha watu wa pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako