• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyaraka muhimu zatangazwa baada ya kufungwa kwa Mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing

    (GMT+08:00) 2018-09-05 10:15:03

    Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofungwa jana hapa Beijing ulitangaza nyaraka mbili muhimu zikiwemo Azimio la Beijing, na Mipango ya utekelezaji, ambazo zimeonesha kwa pande zote maafikiano kati ya China na Afrika kuhusu masuala muhimu duniani kwa hivi sasa. Rais Xi Jinping wa China ameeleza kuwa mkutano wa kilele wa FOCAC wa mwaka huu umefungua ukurasa mpya wa kihistoria wa uhusiano kati ya pande hizo mbili, na kuweka mnara mpya katika ushirikiano kati ya kusini na kusini katika zama mpya.

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa mkutano huo wa FOCAC kwa nyakati tofauti waliendesha mkutano wa viongzoi uliofanyika siku hiyo, na kupitisha nyaraka mbili za matokeo. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika baada ya mkutano huo, rais Xi Jinping anasema:

    "Mkutano huo umetangaza Azimio la Beijing linalohusu kujenga Jumuiya ya karibu zaidi yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika, na kujumuisha maafikiano kati ya pande hizo mbili kuhusu masuala muhimu ya kimataifa na ya kikanda, ambalo limeonesha ishara muhimu ya ushirikiano kati ya China na Afrika katika kutafuta maendeleo ya pamoja. Vilevile mkutano huo umepitisha Mipango ya utekelezaji ya Beijing ya 2019/2020 ambayo imethibitisha kipaumbele cha mipango ya utekelezaji katika sekta nane muhimu katika miaka mitatu ijayo ambayo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali."

    Rais Xi pia ameeleza kuwa, hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa zaidi katika miaka mia moja iliyopita, ncha nyingi zimeibuka duniani huku mafungamano ya kiuchumi yakikuzwa, watu wa nchi mbalimbali wanahusiana kwa karibu zaidi. Kutokana na hali hii, China na Afrika zimeafikiana kujenga Jumuiya ya karibu zaidi yenye hatma ya pamoja. Rais Xi anasema:

    "Tungependa kushirikiana kujenga kwa pamoja Jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika ambayo inabeba majukumu, kufanya ushirikiano, kuendeleza utamaduni, kulinda usalama na kuishi kwa masikilizano kwa pamoja. China na Afrika zinapenda kuimarisha uoanishaji wa mikakati na utaratibu wa sera, kuhimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili kuhusu "Ukanda mmoja, Njia moja", kulinganisha pendekezo la 'Ukanda mmoja, Njia moja' na Ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika, Ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa, pamoja na mikakati ya maendeleo ya nchi mbalimbali za Afrika, kutilia maanani katika kutekeleza mipango ya utekelezaji katika sekta nane kuhusu kuhimiza maendeleo ya viwanda, kuunganisha miundo mbinu, kurahisisha shughuli za biashara, kupata maendeleo yasiyo na uchafuzi wa mazingira, kujenga uwezo wa kujiendeleza, matibabu na afya, mawasiliano ya utamaduni, pamoja na amani na usalama, ili kutoa fursa nyingi zaidi kwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili."

    Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na mwenzake wa Senegal Bw. Macky Sall wamesema, baraza hilo limekuwa jukwaa kubwa linalohimiza maendeleo ya nchi za Afrika katika miaka 18 iliyopita tangu lianzishwe. Rais Ramaphosa anasema:

    "Tunakubali na kuunga mkono pendekezo la 'Ukanda mmoja, Njia moja' lililotolewa na rais Xi ili kukabiliana na changamoto mbalimbali. Pia tunatumai kutumia fursa hii kuhimiza na kuboresha maeneo yanayohitaji kukamilishwa. Tunamshukuru rais Xi na serikali ya China kwa kukusanya fedha kwa Afrika katika sekta muhimu zikiwemo ujenzi wa miundo mbinu, utandawazi wa viwanda, uchumi wa baharini, teknolojia ya sayansi, afya, elimu na mafunzo ya ufundi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako