• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Nigeria wakutana

    (GMT+08:00) 2018-09-05 13:08:06

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na mwenzake wa Nigeria rais Muhammadu Buhari.

    Rais Xi amesema China inakaribisha Nigeria kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuongeza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika ujenzi wa miundombinu, kilimo na uzalishaji viwandani, kuimarisha mawasiliano ya kitamaduni, kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Nigeria na kufanya ushirikiano kati ya China na Nigeria kuwa mfano wa kuigwa wa ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Rais Buhari amepongeza China kwa kufanya kwa mafanikio mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, ambalo litakuwa jukwaa muhimu la kutoa mustakbali mzuri kwa watu bilioni 2.6 wa Afrika na China. Amesema Nigeria inapongeza pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na kulitaja kama ni msingi muhimu kwa pande hizo mbili kupata mafanikio na maendeleo kwa pamoja.

    Baada ya mazungumzo yao, marais hao walishuhudia kusainiwa kwa nyaraka muhimu za ushirikiano wa pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako