• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-05 17:31:57

    Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahammat hapa Beijing.

    Rais Xi Jinping amemshukuru Bw. Faki kwa kutoa mchango muhimu katika kufanikisha mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika hapa Beijing. Anasema:

    "Nimefurahi sana kukutana na Bw. Faki, nakushukuru kwa mchango wako kwa mkutano huo. China siku zote inathamini uhusiano kati yake na Umoja wa Afrika kwenye kiwango cha kimkakati na kwa muda mrefu, na inauunga mkono Umoja wa Afrika kutoa umuhimu wa uongozi katika mchakato wa utandawazi wa Afrika. Katika miaka ya karibuni ushirikiano kati ya China na Afrika umepata mafanikio makubwa, na pande hizo mbili zinafanya mawasiliano na uratibu zaidi katika mambo ya kimataifa."

    Kwa upande wake, Bw. Faki amesifu mkutano wa kilele wa FOCAC, na alikuwa na haya ya kusema:

    "Kwanza nataka kutoa pongezi kwa sababu mafanikio tuliyopatikana jana ni makubwa, aidha mafanikio hayo yatasaidia kuimarisha uhusiano wa urafiki na ushirikiano kati ya Afrika na China."

    Bw. Faki amesema hatuamanane zilizopendekezwa na rais Xi Jinping zinaambatana vizuri na pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja na pia zitausaidia Umoja wa Afrika kutimiza ajenda ya mwaka 2063.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako