• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wakenya kupunguziwa gharama ya umeme

    (GMT+08:00) 2018-09-05 19:50:04

    Wakenya watafurahia kuongezwa kwa megawati 300 kwenye mtambo wa kitaifa wa kuzalisha umeme. Hii ni baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa kawi ya upepo katika eneo la Loiyangalani , Ziwa Turakana. Mradi huu ambao utazinduliwa rasmi mwishoni mwa mwezi huu baada ya kukawia kwa miezi 18, umegharimu takriban shilingi bilioni 28, pesa za Kenya. Akizuru eneo la mradi huu, waziri wa Kawi Charles Keter amesema kuwa wakenya watafaidika pakubwa baada ya mradi huu kukamilika kwa sababu ghrama ya kulipia umeme itapungua. Endapo hili litatimia, basi itakuwa afueni kwa mwananchi wa chini haswa baada ya kuongezeka mkwa bei ya bidhaa muhimu na kupanda kwa gharama ya maisha. Vil vile, ilikuwa ahadi yake rais Uhuru Kenyatta ambaye atazindua mradi huu, kuwa wakenya watafurahia umeme kwa bei ya chini pindi tu miradi yote ya kawi ya upepo itakapokamilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako