• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uagnda: Bei ya nyama yapanda.

    (GMT+08:00) 2018-09-05 19:50:25

    Walaji nyama ya kutoka kampala na maeneo mengine nchini Uganda watalazimika kulipa zaidi ili kufurahia kitoweo hiki. Haya yanajiri baada ya usafirishaji wa wanyama kutoka Ankole kupigwa marufuku na kamishna wa afya ya mifugo kwenye wizara ya Kilimo, mwezi Mei mwaka jana. Hii ni kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa Foot and Mouth.

    Baadhi ya wilaya ambazo zimeathirika na marufuku ya kusafirisha mifugo ni Mbarara, Bushenyi, Isingiro, Ibanda, Sheema na Kiruhura. Ukosefu wa mifugo wa kuchinjwa umesababisha uhaba wa nyama na hivyo kuongezaka kwa bei. Utafiti uliofanywa jijini Kampala na Jinja unaonyesha kuwa bei imepand akutoka shilingi 10,000 hadi 12,000 na 13,000 pesa za Uganda kwa kilo moja ya nyama. Kwa sasa ni wanyama 100 pekee wanaochinjwa kila siku jijini Kampala, kinyume na hapo awali ambapo wanyama 200 walikuwa wakichinjwa kila siku.

    Hata hivyo Uganda huuzia mataifa jirani mifugo na huenda hili limechangia ukosefu wa nyama Uganda. Kwa sasa, bei ya ng'ombe pia imepanda nchini Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako