• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Kiwanda kipya cha sukari kujengwa

    (GMT+08:00) 2018-09-05 19:50:56

    Takriban dollar milioni sita zitatumika kwenye ujenzi wa kiwanda kipya cha sukari katika Wilaya ya Hoima. Kiwanda hiki cha sukari kwa jina Bwendero kinamilikiwa na mfanyi biashara wa kibinafsi na kitakuwa cha 13 nchini Uganda, huku kikitarajiwa kusaga miwa yenye tani 1000 kila siku. Mradi huu upo kwenye shamba lenya ukubwa wa ekari 750, ila bado mmiliki wake anasema kuwa wanahitaji nafais kubwa zaidi ya hii. Baadhi ya viwanda vingine kama vile Atiak, Busia, Kyankwazi na Bushenyi huenda vikaanza kuhudumu hivi karibuni. Hata hivyo uwepo wa viwanda vingi vya sukari unaathiri bei ya miwa na kuikosesha thamani. Licha ya hili, wenyeji wamefurahia hatua hii kwa sababu ya nafasi za ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako