• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Tanzania inahitaji wawekezaji wa kilimo na uvuvi

    (GMT+08:00) 2018-09-05 19:51:26

    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Tanzania inahitaji wawekezaji wakubwa kutoka China ambao watawekeza kwenye viwanda vya mazao ya kilimo, samaki na mifugo.

    Aliyasema hayo, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo wa China, Han Changfu, jijini Beijing.

    Alisema katika kipindi hiki ambacho Tanzania imeamua kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda, China ni nchi sahihi kushirikiana nayo kwa sababu ina wawekezaji wa kutosha.

    Waziri Mkuu alisema Serikali zote mbili, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ziko tayari wakati wowote kuwapokea wawekezaji kutoka China.

    Alisema wawekezaji hao watapatiwa ardhi ya kujenga viwanda ambavyo vitatumia mazao ya kilimo, mifugo na bahari, hasa samaki, ambayo mengi yanapatikana kwa wingi nchini.

    Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema Tanzania inahitaji kupata soko la mbaazi na soya nchini China, ili kuwawezesha wakulima wake kuwa na soko la uhakika la mazao hayo.

    Alisema hivi sasa inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa soko la mazao hayo, baada ya wakulima kuitikia wito wa Serikali wa kuwataka walime mazao hayo kwa ajili ya chakula na biashara.

    Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo wa China alisema nchi yake iko tayari kutoa elimu na mafunzo kwa Watanzania, hasa kwa kuandaa semina zitakazowawezesha washiriki kuongeza ujuzi wao.

    Katika mazungumzo hayo, Tanzania na China zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika maeneo ya uvuvi, ambapo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Rashidi Ali Juma, alitia saini kwa upande wa Tanzania na China iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Eudong Yu . Haiya ni kwa mjibu wa gazeti la Mtanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako