• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Migogoro sekta ya maji.

    (GMT+08:00) 2018-09-05 19:52:13

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Unyunyuziaji, Profesa Kitila Mkumbo, amewataka wanasheria wa Wizara ya Maji na Unyunyuziaji pamoja na taasisi zake kuhakikisha wanasimamia sheria wanazoziweka, ili kuepusha migogoro ambayo inaweza kuisababishia Serikali hasara na kukwamisha maendeleo ya Sekta ya Maji.

    Profesa Mkumbo aliyasema hayo katika mkutano uliowakutanisha wanasheria 36 kati ya 41 kutoka taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Maji na Unyunyuziaji, pamoja na wanasheria wa wizara hiyo uliofanyika jijini Dodoma, wenye lengo la kuboresha utendaji wa wanasheria katika Sekta ya Maji katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango.

    Alisema kama washauri na wasimamizi wa sheria katika Sekta ya Maji, waendelee kusimamia vyema sheria, taratibu na miongozo inayotolewa na Serikali na kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako