• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: VAR kuanza kutumika rasmi Uingereza, FA yataja michezo ya majaribio

  (GMT+08:00) 2018-09-06 09:17:44

  Chama cha soka nchini Uingereza FA kimekubaliana na maoni ya wengi kuhusu matumizi ya VAR uwanjani wakati wa ligi kuu nchini humo.

  Kumekuwa na malalamiko mengi sana kuhusiana na makosa yanayotendeka uwanjani hali ya kuwa mwamuzi hayaoni hivyo walishauri uwepo mfumo wa kuyavumbua makosa hayo kwa kupitia mfumo wa VAR kama ulivyotumika katika michuano ya kombe la Dunia na ukiendelea kutumika katika baadhi ya ligi mbalimbali duniani.

  FA imeridhia kutumia mfumo huo wa VAR katika ligi hiyo kubwa kabisa Duniani katika michezo 15 tu ya ligi lakini sio itatumika muda wote bali itatumika kama kujaribu kwanza katika michezo hiyo huku wakikubali kuujaribu mfumo huu katika baadhi ya michezo katika kombe la Carabao na hata katika baadhi ya michezo katika kombe ya FA Cup,lakini majaribio haya yanatarajiwa kuanza baada ya mapumziko ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako