• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA AFCON 2019: Taifa Stars kuifuata Uganda the Cranes leo mchana

    (GMT+08:00) 2018-09-06 09:18:16

    Kikosi cha wacgezaji 23 wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na viongozi 7 wanatarajia kuondoka leo mchana majira ya saa 7 kwa saa za Afrika Mashariki kuelekea nchini Uganda kwa mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza AFCON dhidi ya timu ya taifa ya Uganda (Uganda the Cranes).

    Akizungumza na vyombo vya habari jana, Nahodha wa timu hiyo Mbwana Samatta amesema utakuwa ni mchezo mgumu kutokana na wachezaji wa timu zote mbili kufahamiana zaidi.

    Naye kocha Emmanuel Amunike amesema anaendelea na maandalizi akiendelea kuangalia mapungufu mbalimbali na kuyafanyia kazi ambapo anaamini kikosi kilichopo huku wachezaji wanaocheza nje wakiwa wameripoti wote.

    Wakati huo huo, Timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars) itakutana na Black Stars ya Ghana katika michuano ya kufuzu kombe la Afrika (AFCON) mwakani bila nyota wao Victor Wanyama ambaye ni majeruhi.

    Kiungo wa Tottenhman ya Uingereza ambaye pia ni nahodha wa Harambee Stars ya Kenya Victor Wanyama ana majeraha ya goti aliyoyapata kwenye ligi kuu ya Uingereza mwezi uliopita.

    Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa Jumamosi wikiendi hii jijini Nairobi. Baada ya kulimana na Ghana, Kenya itacheza mechi ya kirafiki na timu ya taifa ya Malawi septemba 11 katika uwanja wa Kasarani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako