• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI US OPEN: Nadal, Serena watinga nusu fainali

    (GMT+08:00) 2018-09-06 09:18:51

    Mcheza tenisi maarufu upande wa wanaume raia wa Hispania, Rafael Nadal amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya tenisi baada ya kumshinda mpinzani wake, Dominic Thiem.

    Nadal amefanikiwa kushinda mechi hiyo ambayo ilikuwa ndefu kuliko mechi zingine zote za michuano ya mwaka huu kwa jumla ya seti 0-6 6-4 7-5 6-7 (4-7) 7-6 (7-5), mechi ambayo ilitumia masaa 4 na dakika 49 kumalizika.

    Kwa upande wa wanawake, Serena Williams ametinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kumshinda, Karolina Pliskova kwa seti 6-4, 6-3.

    Serena Williams atakutana na Anastasija Sevastova katika hatua ya nusu fainali leo. Sevaskova alimtoa bingwa mtetezi wa michuano hiyo, Sloane Stephens katika hatua ya robo fainali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako