• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Beijing wa FOCAC ni mnara wa historia wa kuhimiza mshikamano, ushirikiano na maendeleo ya pamoja

    (GMT+08:00) 2018-09-06 17:01:17

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo alipohojiwa na waandishi wa habari amesema, mkutano wa 2018 wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC ni shughuli kubwa zaidi ya kidiplomasia iliyoandaliwa na China, na kwenye mkutano huo, China na Afrika zilishirikiana kwa dhati, na kufikia mafanikio mengi yenye maana ya kina. Amesema mkutano huo ni mnara wa historia wa kuhimiza mshikamano, ushirikiano na maendeleo ya pamoja kati ya pande hizo mbili.

    Bw. Wang Yi amesema mafanikio makuu yaliyofikiwa kwenye mkutano huo ni pamoja na China na Afrika kukubali kujenga jumuiya karibu zaidi yenye mustakabali wa pamoja, nchi za Afrika zinaunga mkono na kujiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", Afrika kusifu "hatua nane" zilizotolewa na China kwa ajili ya kuhimiza ushirikiano katika siku zijazo, pande hizo mbili kukubali kushikilia pande nyingi, na kupinga vitendo vy upande mmoja, na kuunga mkono Umoja wa Mataifa.

    Kwenye mkutano huo, China na Afrika zilisaini makubaliano karibu 150 ya ushirikiano, yakiwemo makubaliano kuhusu "Ukanda Mmoja,Njia Moja" yaliyosainiwa kati ya China na nchi 28 za Afrika. Aidha, mkutano huo ulitoa "taarifa ya pamoja ya Beijing kuhusu ujenzi wa jumuiya karibu zaidi yenye mustakabali wa pamoja" na "mpango wa harakati ya Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika kati ya mwaka 2019-2021", na kudhihirisha hatua mpya karibu 100 za kuongeza ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Rais Xi Jinping alitoa hotuba kadhaa muhimu na kufafanua mawazo ya China kuhusu uhusiano kati yake na Afrika, na kutetea China na Afrika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya kubeba majukumu kwa pamoja, kushirikiana na kutafuta mafanikio ya pamoja, kunufaishana, kustawisha utamaduni na kuimarisha usalama kwa juhudi za pamoja, na kuishi pamoja kwa masikilizano. Bw. Wang Yi amesema, rais Xi Jinping alisisitiza China haitafanya mambo matano katika ushirikiano na Afrika, ambayo ni kutoingilia chaguo la nchi za Afrika la kujiendeleza kwa njia inayolingana na hali yao, kutoinglia mambo ya ndani ya nchi hizo, kutozishinikiza kupokea maoni ya China, kutoweka masharti yoyote ya kisiasa wakati inapotoa misaada, na kutojaribu kupata maslahi ya kisiasa inapotoa uwekezaji barani Afrika.

    Aidha, rais Xi alitoa hatua mpya za kuhimiza ushirikiano katika sekta nane za uzalishaji, miundo mbinu, biashara, maendeleo yasiyosababisha uchafuzi, ujenzi wa uwezo, afya, mawasiliano ya watu, na usalama. Bw. Wang anaona hatua hizo ni mafanikio makubwa zaidi yaliyofikiwa kwenye mkutano huo, kwani imepanga njia halisi ya maendeleo ya pamoja ya China na Afrika.

    Mwaka huu, China imeandaa mikutano kadhaa ya kuhimiza ushirikiano kati ya nchi za kusini, yakiwemo mkutano wa kilele wa FOCAC, mkutano wa Ushirikiano kati ya China na Latin-America, mkutano wa ushirikiano kati ya China na nchi za kiarabu, mkutano wa Boao, na mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai. Bw. Wang Yi amesema katika siku zijazo, China itaendelea kuongeza ushirikiano na uratibu wa kimkakati na nchi nyingine zinazoendelea, ili kukabiliana na changamoto kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako