• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC watia nguvu kwa maendeleo ya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-06 18:25:39

    Mkutano wa kilele wa mwaka 2018 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika hapa Beijing umemalizika. Mkutano huo umepitisha azimio la Beijing na mpango wa utekelezaji wa miaka mitatu ijayo, ambao umepongezwa na China, Afrika na hata jumuiya ya kimataifa. Hatua nane zilizotolewa kwenye mkutano huo hakika zitatia nguvu kwa maendeleo mapya ya Afrika.

    Hatua hizo nane zinatupia macho mahitaji ya Afrika na uwezo wao, yaani kuweka mkazo katika kuimarisha ushirikiano katika kuhimiza maendeleo ya viwanda, kuunganisha miundombinu, kurahisisha biashara, kuleta maendeleo bila ya kuchafua mazingira, kujenga uwezo, afya na matibabu, mawasiliano ya utamaduni, na amani na usalama.

    Hatua hizo zinaendana na mahitaji ya Afrika, na zitasaidia bara hilo kutimiza malengo ya maendeleo. Hatua za ushirikiano na Afrika zilizotolewa na China zinaendana na sekta zinazopewa kipaumbele za maendeleo ya uchumi na jamii barani Afrika. Kutokana na hilo mkurugenzi wa idara ya Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika ya kituo cha maendeleo cha shirika la ushirikiano wa uchumi OECD Bw. Arthur Minsat amesema, pendekezo la hatua nane litasaidia kuhimiza kiwango cha viwanda na elimu cha Afrika, na kusaidia Umoja wa Afrika kutimiza ajenda ya mwaka 2063.

    Mkutano huo utainua imani ya waafrika kuhusu mustakabali wa maendeleo ya Afrika. Kutokana na historia ya ukoloni barani Afrika, Waafrika wanatamani kutimiza maendeleo endelevu, lakini wana shaka juu ya namna ya kutimiza lengo hilo. Tangu mwaka 2000 Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika lilipoanzishwa, China siyo tu inaleta soko, fedha na teknolojia barani Afrika, bali pia inatoa uzoefu wa maendeleo kwa Afrika, mambo hayo yanaimarisha imani ya nchi za Afrika kutafuta mfumo wa kujiendeleza unaoendana na hali yao yenyewe. Kwenye mkutano huo, rais Xi Jinping wa China amesema maendeleo ya Afrika hayana mpaka, na kwamba Afrika ina mustakabali mzuri sana. Maneno hayo yanawatia moyo Waafrika, pia yanatia moyo kwa watu wote duniani wanaofuatilia Afrika.

    Mkutano huo umeongeza uelewa wa dunia juu ya Afrika, na kuhimiza jumuiya ya kimataifa kuongeza uwekezaji na ushirikiano na Afrika. Kwa sasa Afrika ni sehemu nyeti inayoshirikiana na nchi nyingi, nchi mbalimbali zimeanza kufanya ushirikiano wa mambo ya diplomasia na uchumi na Afrika, na bara la Afrika limekuwa sehemu inayovutia uwekezaji wengi duniani. Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema, ushirikiano kati ya China na Afrika umeleta mabadiliko makubwa kwa Afrika, pia umebadilisha hadhi ya Afrika duniani.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, Afrika kudumisha amani na utulivu na kutimiza maendeleo endelevu ni mambo muhimu yanayozingatiwa na Umoja wa Mataifa katika kuhimiza amani na maendeleo. Ushirikiano kati ya China na Afrika unaojengwa juu ya kanuni ya kunufaishana, unafanya kazi muhimu kwa maendeleo ya Afrika. Mkutano wa kilele wa mwaka huu wa FOCAC ni mwanzo mpya wa ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako