• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China itachukua hatua za kukabiliana na Marekani kama itaongeza ushuru mpya kwa bidhaa za China

    (GMT+08:00) 2018-09-06 19:20:20

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, China italazimika kujibu endapo Marekani itachukua hatua yoyote mpya ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China.

    Bw. Gao Feng amesisitiza kuwa, vita ya kibiashara haisaidii kutatua suala lolote, na mazungumzo ya usawa na uaminifu ndio chaguo sahihi la kutatua mgogoro wa biashara kati ya China na Marekani. Amesema China itafuatilia kwa karibu athari mbalimbali zinazosababishwa na kuongeza ushuru, na kuchukua hatua kusaidia kampuni zake kukabiliana na athari hizo. Bw. Gao ameongeza kuwa, China ina imani, uwezo na njia ya kulinda utulivu na maendeleo mazuri ya uchumi.

    Habari zinasema, Marekani itakamilisha muda wa kukusanya maoni ya watu kuhusu kuongeza ushuru wa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200. Zaidi asilimia 90 ya watu wanaotoa maoni wanapinga hatua hiyo, lakini serikali ya Marekani inapanga kuendelea kuchukua hatua hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako