• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Wafanyibiashara nchini Uganda wahofia utekelezaji wa marufuku ya mifuko ya plastiki

    (GMT+08:00) 2018-09-06 19:33:09

    Kampuni za kutengeneza plastiki zimeanza kuingia na wasi wasi baada ya serikali kusisitiza kusimamishwa utengenezaji wa mifuko ya plastiki.

    Baada ya Rwanda na Kenya kushirikiana kutekeleza marufuku hayo,Uganda nayo imeanza hatua za kwanza kutaka marufu ya mifuko hiyo kutekelezwa.

    Sheria ya mwaka 2009 ya fedha inapiga marufuku utengenezaji, uuzaji na utumiaji wa mifuko na magunia ya plastiki kuanzia Machi 31, mwaka 2010 lakini biashara na matumizi nchini Uganda ni kama kawaida.

    Baadhi ya wafanyibiashara wa Uganda wamekua wakipata fedha nyingi kwa kuuza mifuko hiyo baada ya wakenya kuinunua na kuiingiza nchini kwa njia ya ulanguzi.

    Makampuni ya kutengeneza mifuko hiyo yamelalamika kuwa hawajapewa njia mbadala ya bidhaa zitakazotumika kubebea vitu madukani na sokoni.

    Kenya ilipewa tuzo na Umoja wa mataifa kwa juhudi zake za kutekeleza marufu hayo mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako