• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-09-06 20:56:56

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na waziri mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa.

    Rais Xi amesema, China na Tanzania zimedumisha urafiki kwa muda mrefu, inatilia maanani maendeleo ya uhusiano kati yake na Tanzania, na inapenda kuongeza ushirikiano wa kirafiki katika sekta mbalimbali ili kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili. Ameongeza kuwa China itashirikiana na Tanzania kuhimiza uhusiano kati yao na uhusiano kati ya China na Afrika kuendelea kwa kutumia nafasi ya kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa kilele wa Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Beijing.

    Naye Bw. Majaliwa amesema, hotuba ya rais Xi kwenye ufunguzi wa mkutano wa FOCAC wa Beijing ni moja ya hotuba bora zaidi kuhusu ushirikiano wa kimataifa katika karne ya 21, mawazo na hatua nane zilizotolewa na China kuhusu ushirikiano vinalingana na mahitaji ya maendeleo ya Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako