• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kufuzu AFCON 2019: Taifa Stars yawasili Uganda tayari kuvaana na Uganda the Cranes, Amavubi wawasubiri Ndovu wa Ivory Coast

  (GMT+08:00) 2018-09-07 09:21:47

  Timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wamewasili salama nchini Uganda jana kwa ajili ya mchezo wa kundi L kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya wenyeji Uganda the Cranes, Taifa Stars inaongozwa na nahodha wake Mbwana Samatta ambaye anakipiga katika klabu ya KRC Genk. mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Namboole kesho Jumamosi mjini Kampala.

  Nayo timu ya taifa ya Rwanda (Amavubi) iko kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wake dhidi ya Ndovu ya Ivory Coast mchezo utakaochezwa Jumapili uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali Rwanda.

  Ni katika kusaka tiketi ya kushiriki kombe la Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon. Ni mechi ya pili kwa kila upande, Rwanda ilipoteza mechi ya kwanza dhidi Jamuhuri ya Afrika ya kati.Ivory Coast walijipatia pointi 3 dhidi ya Gunea.

  Jijini Nairobi: Black Stars ya Ghana tayari imetua nchini Kenya kukabiliana na Harambee Stars ya Kenya katika mechi ya kundi F ya kufuzu kushiriki kombe la Afrika (AFCON 2019). Mechi hiyo itachezwa kesho jumamosi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako