• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Tanzania kuwa mwenyeji wa mbio za nyika

    (GMT+08:00) 2018-09-07 09:23:28

    Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya mbio za yyika Afrika zinazotarajiwa kufanyika mwaka 2020.

    Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa shirikisho la riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday, amesema Tanzania itanufaika katika sekta ya utalii kupitia mashindano hayo.

    Gidabuday ameeleza kuwa, Shirikisho la Kimataifa (IAAF) na Afrika (CAAA) limeichagua Tanzania, baada ya kuvutiwa na amani na utulivu.

    Hii itakuwa mara ya kwanza Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa kwa IAAF na CAAA imewahi kuandaa mashindano ya vijana Afrika Mashariki na Kati (EAAR).

    Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika mikoa ya Kaskazini kutokana na uwepo mbuga nyingi za wanyama ambazo ni sehemu kubwa ya vivutio vya utalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako