• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya biashara ya China kuchukua hatua kuhimiza maendeleo ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-07 16:16:19

    Mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC umefikia matokeo kadhaa ya kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara. Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, China itachukua hatua mbalimbali kutekeleza ushirikiano wa sekta za uwekezaji, uchumi na biashara kati yake na nchi mbalimbali za Afrika.

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, China itafanya uvumbuzi wa mfumo wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati yake na Afrika, kuanzisha maonyesho ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika, kujenga dirisha jipya la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati yake na Afrika hasa katika sehemu mbalimbali za China, kuimarisha ujenzi wa maeneo ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, kuunga mkono makampuni mbalimbali ya China kujenga maeneo ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara yenye faida nzuri kwa jamii na kwa uchumi, kuhamasisha makampuni ya China kupanua uwekezaji barani Afrika, na kutoa uungaji mkono na msaada zaidi kwa makampuni ya China kuwekeza barani Afrika. Pia amesema China itatumia fursa ya maonyesho kimataifa ya bidhaa kutoka nje ya China, maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa na China na utaratibu wa ushirikiano wa biashara ya kielekitroniki ili kuhimiza maendeleo ya biashara kati yake na Afrika.

    "China itatumia vya kutosha jukwaa la maonyesho ya kimataifa ya bidhaa kutoka nchi za nje ya China, kusukuma mbele uuzaji wa bidhaa za nchi za Afrika nchini China. China itaunga mkono mashirikisho ya wafanyabiashara ya China na makampuni ya China kwenda Afrika kuendesha maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa na China kila mwaka, na kupeleka bidhaa nzuri za China barani Afrika, pia kuunga mkono nchi za Afrika kufanya shughuli mbalimbali za kuhimiza biashara. China itajadiliana na nchi husika za Afrika kuanzisha utaratibu wa ushirikiano wa biashara ya kielekitroniki, kuimarisha ushirikiano katika uratibu wa sera, kuunganisha mpango, kupeana uzoefu, utafiti wa pamoja na kuwaandaa watu."

    Habari nyingine zinasema, mazungumzo ya mkataba kuhusu biashara huria kati ya China na Mauritius yamekamilika tarehe 2. Mkataba huo ni mkataba wa kwanza wa biashara huria uliofikiwa kati ya China na nchi za Afrika. Bw. Gao Feng amesema kuwa, makubaliano hayo yanahusu biashara ya bidhaa, biashara ya huduma, uwekezaji, ushirikiano wa uchumi na sekta nyingine nyingi. Amesema kufikiwa kwa mkataba huo kutazidisha uhakikisho wenye nguvu zaidi kwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Mauritius. Pia China itaendelea kufanya mazungumzo ya mkataba wa biashara huria pamoja na nchi nyingine za Afrika zenye nia hiyo, ili kuweka mazingira mazuri zaidi kwa ajili ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako