• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni binafsi za safari ya anga ya juu zaendelea kwa kasi nchini China

    (GMT+08:00) 2018-09-07 16:38:50

    Kampuni binafsi ya Xingji Rongyao ya safari ya anga ya juu jumatano wiki hii ilirusha satilaiti tatu kwenye anga ya juu ya ngazi ya chini kwa roketi iliyobuniwa na kampuni hiyo.

    Hii ni mara ya pili kwa kampuni binafsi ya China kurusha satilaiti ya kibiashara baada ya kampuni ya Lingyi Kongjian kufanya hivyo kwa mara ya kwanza mwezi Mei mwaka huu, ikiashiria maendeleo ya kasi ya kampuni binafsi za safari ya anga ya juu nchini China. Kampuni hizo zinafanya utafiti wa roketi zinazoweza kurusha satelaiti kwenye anga ya juu kwa kuwa satelaiti za sasa hazina uwezo wa kuzunguka sayari ya dunia.

    Tovuti ya mtandao wa Internet ya kampuni ya Xingji Rongyao inaonesha kuwa kampuni hiyo inabuni roketi inayoweza kutumiwa kwa marudio, na injini ya roketi inayotumia hewa ya Methane ambayo ni ya kisasa zaidi na pia ni vigumu zaidi kutengenezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako