• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China kuhudhuria baraza la 4 la uchumi la mashariki nchini Russia

    (GMT+08:00) 2018-09-07 18:12:45

    Msaidizi wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhang Hanhui amesema rais Xi Jinping wa China anatarajiwa kwenda nchini Russia ambapo atahudhuria mkutano wa baraza la nne la uchumi la mashariki utakaofanyika mjini Vladivostok nchini Russia.

    Bw. Zhang Hanhui amesema, baraza hilo lililoanzishwa kutokana na pendekezo la rais Vladmir Putin wa Russia, ni hatua muhimu ya kuhimiza ushirikiano wa Russia na nchi za mashariki ya mbali. Hii ni mara ya kwanza ya rais wa China kuhudhuria baraza hilo, ambapo anatarajiwa kufanya mawasiliano wa urafiki na viongozi wa nchi husika watakaohudhuria baraza hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako