• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasaini makubaliano na nchi 37 za Afrika na Umoja wa Afrika kuhusu pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja

    (GMT+08:00) 2018-09-07 18:21:42

    Naibu mkuu wa idara ya ushirikiano wa kimataifa ya kamati ya mageuzi na maendeleo ya taifa ya China Bw. Xia Qing amesema mpaka kufikia jana, China imesaini makubaliano na nchi 37 za Afrika na Umoja wa Afrika kuhusu kujenga miradi ya Ukanda Mmoja na Njia Moja kwa pamoja.

    Bw. Xia amesema idadi ya nchi zilizosaini makubaliano hayo imechukua asilimia 70 ya nchi 53 zilizohudhuria mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC. Ameongeza kuwa, China itaendelea kuwasiliana na nchi husika za Afrika na kuhimiza kusaini makubaliano na nchi nyingi zaidi kuhusu ushirikiano wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, ili kutimiza lengo la kuzishirikisha nchi zote barani Afrika. Pia itasukuma mbele ushirikiano katika sekta mbalimbali, kufanya juhudi kupata mafanikio ili kunufaisha nchi na watu wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako