• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi atuma barua ya kupongeza maonyesho ya uwekezaji na biashara

    (GMT+08:00) 2018-09-08 16:13:49

    Rais Xi Jinping ametuma barua ya kupongeza maonyesho ya kimataifa ya uwekezaji na biashara ambayo yalifunguliwa kwenye mji wa mashariki ya China wa Xiamen katika jimbo la Fujian.

    Katika barua hiyo, Rais Xi amesema kwa zaidi ya miaka 20, maonyesho hayo yameshikilia msimamo wa kutengeneza majukwaa kwa ajili ya kukuza uwekezaji kwa njia mbili ambazo kutoa taarifa rasmi, na majadiliano kuhusu namna za uwekezaji.

    Aidha, Rais Xi amesema maonyesho hayo yamekuwa moja ya matukio ya kimataifa ya uwekezaji yenye ushawishi mkubwa duniani, na yamekuwa na mchango chanya katika utekelezaji wa sera ya China ya kufungua mlango, pamoja na mchakato wa kuufanya ujamaa kuwa kisasa. Akisema ikiwa sasa ni mwaka wa 40 tangu kuanza utekelezaji wa sera ya mageuzi na kufungua mlango, hivyo China itaendelea kufungua zaidi na zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako