• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni binafsi ya China yaonyesha nia ya kugeukia fursa za soko la Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-09 17:37:46

    Katika mkutano mkuu wa uwekezaji na biashara kati ya China na Afrika uliofanyika mjini Hangzhou, huko Zhejiang mashariki ya China, makampuni binafsi kutoka China yameanza kuonyesha nia ya kutaka kuwekeza barani Afrika.

    Mwezi uliopita kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing, Naibu Waziri wa biashara wa China Qiang Keming alisema uwekezaji katika sekta binafsi nchini China umeongezeka kwa kasi na ndio sababu kubwa inayofanya taifa la China lipate nguvu kubwa ya kutaka kuwekeza barani Afrika.

    Takwimu zinaonyesha kuwa makampuni ya China yaliyowekeza Afrika ni zaidi ya 10,000, na kuna uwezekano mkubwa idadi hiyo ikaongezeka zaidi katika kipindi cha miaka 15 au 20 ijayo.

    Uwekezaji huo wa kibiashara kati ya China na Afrika hadi kufikia mwaka 2017 ulikuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 170 ikiwa ni ongezeko la asilimia 14 ikilinganishwa na mwaka mmoja kabla.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako