• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta za utamaduni na utalii kuwa msukumo mpya wa uchumi wa Tibet

    (GMT+08:00) 2018-09-10 17:21:59

    Hafla ya kusaini mkataba wa kukuza uwekezaji katika mkoa unaojiendesha wa Tibet imefanyika mjini Lhasa wakati wa mkutano wa nne wa maonyesho ya Tibet.

    Katika mkutano huo, miradi 108 yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 8 imesainiwa, ikiwemo miradi 17 yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.7 ya sekta za utamaduni na utalii ambayo inachukua zaidi ya asilimia 20 ya thamani ya jumla makubaliano yaliyosainiwa katika mkutano huo.

    Mwaka jana, thamani ya sekta ya utamaduni mkoani Tibet imezidi dola za kimarekani milioni 600, huku mapato ya utalii yakifikia dola za kimarekani milioni 822, na sekta hizo mbili zimekuwa msukumo mpya wa ukuaji wa uchumi wa Tibet

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako