• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Oparesheni dhidi ya pombe bandia yaanza

    (GMT+08:00) 2018-09-10 20:27:24

    Bodi ya ubora wa bidhaa nchini Rwanda imeanzisha oparesheni dhidi ya wafanyibiashara wanaouza pombe bandia.

    Mkurugenzi wa bodi hiyo Philip Nzaire amesema oparesheni hiyo imefanywa katika maeneo ya Kimisagara na Muhimana huku zaidi ya lita elfu 6 za pombe hiyo zimekamatwa .

    Pombe hiyo ya thamani ya franki milioni 3 imetengenezwa na bidhaa ambazo sio sahihi kwa mujibu wa ukaguzi wa maafisa wa idara ya afya.

    Wafanyibiashara wa pombe haramu wameonywa kwamba oparesheni hiyo itaendelea kote nchini Rwanda .

    Hatua hii inajiri baada ya malalamishi ya watu wa Rwanda kupata maradhi nawengine kupoteza uwezo kuona baada ya kutumia pombe iliyotengenezwa na kemikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako