• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, kuelekea uchaguzi mkuu Simba, 21 wajitokeza kuwania uongozi

    (GMT+08:00) 2018-09-11 09:11:09

    Kuelekea uchaguzi mkuu wa viongozi wa moja ya klabu kongwe ya soka barani Afrika, Simba ya Tanzania utakaofanyika Novemba 3, jumla ya watu 21 wamechukua fomu ili kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

    Kati yao, wawili pekee ndiyo wanaowania nafasi ya Urais wa klabu, Mtemi Ramadhani na Swedi Nkwabi,na wengine 19 wanawania nafasi ya ujumbe klabuni hapo.

    Licha ya kudaiwa kumudu uongozi wa klabu hiyo, kaimu Rais wa klabu hiyo kwa sasa, Salim Abdallah anadaiwa kujiweka kando.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako