• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, TFF yamuadhibu kiongozi wa klabu kwa kosa la kuhujumu timu ya taifa

  (GMT+08:00) 2018-09-11 09:11:39

  Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF limetoa adhabu kwa meneja wa klabu ya Simba aitwaye Robert Richard ya kutojihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha mwaka mmoja kutokana na makosa mawili ya ukosefu wa maadili.

  Kosa la kwanza inadaiwa ni kuhujumu timu ya Taifa ya Tanzania kupitia wachezaji, na kosa la pili ni kitendo cha dharau kwa mamlaka hiyo.

  Pamoja na adhabu hiyo, kiongozi huyo pia anapaswa kulipa faini ya fedha za Tanzania shilingi Milioni 4 kutokana na makosa hayo mawili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako