Goli la Ureno lilifungwa na Andre Silver kunako dakika ya 48 ya mchezo huo, na katika mechi nyingine zilizochezwa jana Sweden ikiwa nyumbani jana imefungwa magoli 3-2 na Uturuki.
Scotland nayo imeanza vyema mashindano hayo kwa kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Albania, Monteenegro ikishinda 2-0 ilipocheza na Lithuania, Serbia na Romania zikitoka sare ya 2-2, na sare nyingine zikiwa ni 1-1 kati ya Andorra na Kazakhistan, 1-1 Malta na Azerbaijan.
Lakini mambo yalikuwa mazuri kwa timu ya Kosovo ambapo mchezaji wao wa kutegemewa Atdhe Nahiu anayecheza klabu ya Sheffield Wednesday ya Uingereza alifunga magoli yote mawili ya ushindi wa 2-0 timu hiyo ilipokuwa nyumbani kucheza na timu ya taifa ya visiwa vya Feroe.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |